TIMU ya Manchester United itamenyana na wapinzani wengine wa Hispania, Sevilla katika Robo Fainali ya Europa League baada ya kuzitoa Barcelona na Real Betis mfululizo kwenye hatua zilizopita.
Mechi nyingine za Robo Fainali ni Juventus dhidi ya Sporting Lisbon, Bayer Leverkusen na Union SG na Feyenoord watacheza na AS Roma ya kocha Jose Mourinho.
Man United ikifuzu mbele ya Sevilla katika Nusu Fainali itakutana na mshindi kati ya Juventus na Sporting Lisbon iliyoitoa Arsenal.
Mshindi baina ya Bayer Leverkusen na Union SG atamenyana na mshindi kati ya Feyenoord watacheza na AS Roma, wakati Fainali itapigwa Mei 31 Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest nchini Hungary.
0 comments:
Post a Comment