WENYEJI, Liverpool wamewaadhibu pasi na chembe ya huruma mahasimu wao, Liverpool kwa kuwatandika mabao 7-0 leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Cody Gakpo dakika ya 43 na 50, Darwin Nunez dakika ya 47 na 75, Mohamed Salah dakika ya 66 na 83 na Roberto Firmino dakika ya 88.
Kipigo hicho kinakuja wakati mashabiki wa Manchester United wamekwishaanza kujenga imani na kocha Mholanzi, Erik ten Hag baada ya kuipa timu taji la Carabao na kuiweka ndani ya Nne Bora timu kwenye Ligi Kuu kwa muda mrefu.
Kwa ushindi huo, Liverpool ambayo ilikwishaanza kupoteza makali chini ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp inafikisha pointi 42 na kusogea nafasi ya tano, ikizidiwa pointi saba na Man United baada ya wote kucheza mechi 25.
0 comments:
Post a Comment