NAHODHA Harry Kane jana ameweka rekod ya kuwa mfungaji wa mabao mengi kwenye kikosi cha England baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Italia kwenye mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2024 Uwanja wa Diego Armando Maradona Jijini Napoli.
Kane alifunga bao lake kwa penalti 44 ambalo lilikuwa la pili baada ya Declan Rice kufunga la kwanza dakika ya 13, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Mateo Retegui dakika ya 56.
Katika mchezo huo England ilimaliza pungufu kufuatia Luke Shaw kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 80.
Na kwa kufunga jana, Kane amefikisha mabao 54 na kumpiku aliyekuwa anaongoza kwa ufungaji wa mabao mengi England, Wayne Rooney (53) na wote wanafuatiwa Sir Bobby Charlton (49), Gary Lineker (48) na Jimmy Greaves (44).

0 comments:
Post a Comment