MWANASHERIA Gianni Infantino (52) amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kipindi cha miaka mingine minne katika uchaguzi uliofanyika leo Jijini Kigali nchini Rwanda.
Mzaliwa huyo wa Uswisi mwenye uraia wa Italia pia kwa sababu ya wazazi wake, aliingia madarakani FIFA Februari 26, mwaka 2016 akichukua nafasi ya Mcameroon Issa Hayatou aliyekuwa anakaimu kufuatia kuondolewa madarakani kwa Sepp Blatter kwa kashfa ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi.
Blatter, naye Mswisi aliyeingia madarakani Juni mwaka 1998 kuchukua nafasi ya Mbrazil, João Havelange, Desemba 21 mwaka 2015 alifungiwa miaka minane kujihusisha na soka kabla ya adhabu yake kupunguzwa hadi miaka sita Februari mwaka 2016.
Infantino hakuwa na upinzani katika uchaguzi wa leo na kwa sasa atakuwa madarakani hadi mwaka 2027 na anaweza kuendelea na kuongoza hadi mwaka 2031 kwa mujibu wa Katiba ya FIFA.
0 comments:
Post a Comment