KOCHA wa Ufaransa, Didier Deschamps amemteu Kylian Mbappe kuwa Nahodha mpya wa timu yake ya taifa.
Uteuzi huo unakuja kuelekea mechi ya kufuzu Euro 2024 dhidi ya Uholanzi baada ya kujiuzulu kwa kipa Hugo Lloris kufuatia Fainali za Kombe la Dunia Ijumaa pale Stade de France.
Nahodha wa zamani, Lloris alijiuzulu soka ya kimataifa baada ya Ufaransa kufungwa kwa penalti 4-2 na Argentina kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Qatar Desemba 18 kufuatia sare ya 3-3.
Tayari Mbappe amepewa Unahodha wa klabu yake, PSG na bila shaka hiyo imemsukuma Deschamps kumpa jukumu hilo na timu ya taifa, ingawa awali ilielezwa angemteua kipa wa AC Milan, Mike Maignan.
0 comments:
Post a Comment