WENYEJI, Manchester United wametoa sare ya 0-0 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Ilikuwa siku ngumu kwa Man United baada ya kiungo wake Mbrazil, Casemiro kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 34 kufuatia kumchezea rafu Carlos Alcaraz wa Southampton.
Man United wanafikisha pointi 50 katika mchezo wa 26, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi 11 na mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
Kwa upande wao, Southampton hali inazidi kuwa mbaya wakiendelea kushika mkia kwa pointi zao 22 za mechi 26.
0 comments:
Post a Comment