TIMU ya Sporting Lisbon imeitupa nje ya michuano ya UEFA Europa League Arsenal kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mchezo wa kwanza timu zilifungana mabao 2-2 nchini Ureno na zikatoka sare ya 1-1 London, Arsenal ikitangulia kwa bao la Granit Xhaka dakika ya 19, kabla ya Pedro António ‘Pote’ kuisawazishia Sporting Lisbon dakika ya 62.
Katika mikwaju ya penalti shuti la Gabriel Martinelli liliokolewa na kipa, Antonio Adan na huo ikawa mwisho wa Arsenal huku Sporting Lisbon ikitinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment