WENYEJI, Arsenal wametoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Bournemouth walitangulia kwa mabao ya Philip Billing sekunde ya 9.11 ya dakika ya kwanza tu ambalo linaweka rekodi ya bao la pili la mapema zaidi katika historia ya Ligi Kuu na Marcos Senesi aliyefunga la pili dakika ya 57.
Arsenal ikazinduka kwa mabao ya Thomas Partey dakika ya 62, Ben White dakika ya 70 na Reiss Nelson dakika ya saba ya muda wa nyongeza baada ya kutimia 90 za kawaida.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 63 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 26, wakati Bournemouth inaendelea kushika mkia na pointi zake 21 za mechi 25.
0 comments:
Post a Comment