MABINGWA wa Tanzania, Young Africans SC wameanza vibaya hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 2-0 na wenyeji, US Monastirienne leo Uwanja wa Olimpiki Hammadi Agrebi Jijini Radès, Tunis nchini Tunisia.
Mabao ya Monastir leo yamefungwa na beki Mtunisia, Mohamed Saghraoui dakika ya 10 na mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Boubacar Traoré dakika ya 16, wote wakimalizia mipira ya kutenga ya kiungo Mfaransa, Haykeul Chikhaoui.
Mechi nyingine ya Kundi D leo, wenyeji, TP Mazembe wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Bamako Jijini Lubumbashi.
Mechi zijazo, Yanga watakuwa wenyeji wa TP Mazembe Jijini Dar es Salaam na Monastir watawafuata Real Bamako nchini Mali.
0 comments:
Post a Comment