MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamepata ushindi wa kwanza katika mechi za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya saba, kiungo Mzanzibari Mudathir Yahya dakika ya 11 na winga Mkongo, Tuisila Kisinda dakika ya 90 na ushei, wakati la Mazembe limefungwa na Alex Ngonga kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 80.
Yanga SC inaokota pointi tatu za kwanza katika kundi hilo baada ya kuchapwa 2-0 kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita na wenyeji, Monastir nchini Tunisia, wakati Mazembe inapoteza mechi ya kwanza ikitoka kushinda 3-1 nyumbani dhidi ya Real Bamako ya Mali.
Mechi nyingine ya Kundi D leo, Real Bamako imelazimishwa sare ya 1-1 na Monastir Jijini Bamako nchini Mali.
Monastir inaendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi zake nna ikifuatiwa na Yanga na Mazembe zenye pointi tatu kila moja, wakati Real Bamako yenye pointi moja inashika mkia.
Mechi zijazo, Februari 26 Yanga watakuwa wageni wa Real Jijini Bamako na Mazembe watawakaribisha Monastir Jijini Lubumbashi.

0 comments:
Post a Comment