• HABARI MPYA

        Monday, January 16, 2023

        TANZANIA PRISONS YASAJILI WATANO DIRISHA DOGO


        KLABU ya Tanzania Prisons imesajili wachezaji watano wapya katika dirisha hili dogo ili kukiongezea nguvu kikosi chake kuelekea simu iliyobaki ya msimu.
        Hao ni kipa Benedict Tinocco aliyesaini miaka miwili, viungo Mohamed Ibrahimu ‘Mo’ mwaka mmoja na nusu, Shaaban Kisiga mwaka mmoja, Lambert Charlse Sabiyanka na winga Meshack Suleiman kutoka Nyasa Big Bullets ya Malawi aliyesaini miaka mitatu.
        Aidha, Tanzania Prisons imewatakia kila la heri wachezaji walioondoka, kipa Hussein Abel na kiungo Mudathir Abdallah.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YASAJILI WATANO DIRISHA DOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry