WENYEJI, Manchester United jana wamefanikiwa kwenda Raundi ya Tano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Reading Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Mabao ya Man United yalifungwa na Wabrazil, Casemiro mawili dakika ya 54 na 58 na Fred dakika ya 66, wakati bao pekee la Reading lilifungwa na beki Msenegal, Amadou Salif Mbengue dakika ya 72.
0 comments:
Post a Comment