WENYEJI, Coastal Union wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Kwa matokeo hayo katika mchezo wa 20 kwa timu zote, Coastal Union wanafikisha pointi 18, ingawa wanabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 na Ruvu Shooting wanafikisha pointi 14 na wao wanaendelea kushika mkia.
0 comments:
Post a Comment