• HABARI MPYA

        Tuesday, January 24, 2023

        AL HILAL YAJA NCHINI KUCHEZA NA AZAM, NAMUNGO NA SIMBA SC


        KLABU ya Al Hilal ya Sudan inatarajiwa kuwasili nchini kesho kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
        Ikiwa nchini, Al Hilal itacheza mechi tatu za kirafiki ikiwemo dhidi ya wenyeji wao, Simba SC Februari 5, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
        Kabla ya hapo, Hilal itacheza 
        Namungo FC Januari 26 na Azam FC Januari 31 katika mechi nyingine mbili za kirafiki Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.


        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: AL HILAL YAJA NCHINI KUCHEZA NA AZAM, NAMUNGO NA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry