MWENYEKITI wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya ametoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Ilala.
Alitoa fedha hizo wakati alipokuwa anafunga kozi ya makocha CAF diploma D iliyokuwa ikiendeshwa makao makuu ya Chama cha soka mkoa wa Ilala (IDFA).
Aliwataka makocha hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kupitia kozi hiyo ambayo ilishirikisha makocha 30 ambalo kati yao Wanaume ni 26 na Wanawake 4.
"Ninawapongeza washiriki wote ambao mmehitimu kozi hii naamini mtakwenda kufanya kazi kwa bidii Mkufunzi aliyewafundisha sina wasi wasi naye,alisema Nyambaya.
Kwa upande wa Mkufunzi wa kozi hiyo Mohamed Tajdeen alisema kuwa kozi hiyo itawasaidia washiriki hao kufundisha timu za kuwanna Ligi Daraja la 3 na Ligi Daraja la 4.
"Kozi hii inawajengea uwezo wa kufundisha mpira na kwa wale watakaofaulu watakuwa na uwezo wa kujiunga na mafunzo ya CAF diploma C,alisema Tajdeen.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku kumi. Mmoja wa washiriki ni Kaimu Katibu Mkuu Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Ramadhan Msilu , alisema licha ya kuwa kiongozi wa mkoa ameamua kujiunga kupata mafunzo hayo ushiriki wake na viongozi wengine ni kuwapa hali washiriki wengine.
0 comments:
Post a Comment