• HABARI MPYA

        Sunday, October 23, 2022

        MAN UNITED YAPATA SARE YA 1-1 KWA CHELSEA


        TIMU ya Manchester United jana imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
        Chelsea walitangulia kwa bao la penalti la Jorginho dakika ya 87 kufuatia Scott McTominay kumchezea rafu Armando Broja, lakini Casemiro akaisawazishia Man United dakika ya 90 na ushei.
        Kwa matokro hayo, Chelsea inafikisha pointi 21 katika nafasi ya nne, ikiizidi pointi moja tu Manchester United baada ya wote kucheza mechi 11.
          
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MAN UNITED YAPATA SARE YA 1-1 KWA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry