TIMU ya Azam FC imeanza vibaya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, Al Akhdar katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza leo Uwanja wa Uwanja wa Februari Jijini Benghazi nchini Libya.
Mabao ya Al Akhdar yamefungwa na Muhiib Seleman kwa penalti dakika ya 11 na Omar Tawrighi dakika ya 37 na 43, kabla ya kipa wa Azam FC, Mcomoro Ali Ahamada kuokoa penalti nyingine dakika ya 90 na ushei.
Timu hizo zitarudiana Oktoba 16, yaani Jumapili ijayo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mshindi wa jumla atasonga mbele.
Mshindi atakwenda kumenyana na moja ya timu zitakazotolewa Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kucheza Hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
0 comments:
Post a Comment