KLABU ya Azam FC imeachana na kocha wake Mfaransa, Denis Lavagne baada ya mwezi mmoja na ushei tangu aajiriwe.
Hatua hiyo inakuja baada ya Azam FC kuchapwa 2-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Ijumaa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Lavagne mwenye leseni ya UEFA Pro, alijiunga na Azam FC Septemba 2, mwaka huu akichukua nafasi ya Msomali, Abdihamid Moalin aliyefukuzwa mwishoni mwa mwezi Agosti.
Sasa timu itakuwa chini ya Muingereza mwenyeji nchini, Kali Ongala na Waspaniola, Dani Cadena kocha wa makipa, Mikel Guillen kocha wa Fiziki na mtaalamu wa tiba za wanamichezo (physio), Mreno Joao Rodrigues.
0 comments:
Post a Comment