BAO pekee la Abalkassim Suleiman dakika ya 48 limetosha kuipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting ya kocha Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi sita katika nafasi ya saba, wakati Polisi inabaki na pointi zake mbili baada ya wote kucheza mechi nne.
0 comments:
Post a Comment