BONDIA Oleksandr Usyk amefanikiwa kutetea mataji yake ya WBA, IBO, WBO na IBF uzito wa juu baada ya kumshinda tena kwa pointi, Muingereza Anthony Joshua usiku wa jana mjini Jeddah, Saudi Arabia.
Majaji wawili walimpa ushindi Usky, Ukraine alimpa pointi 116-112, Muingereza akampa 115-113 huku Mmarekani akimpa ushindi Joshua wa pointi 115-113. Baada ya pambano, Joshua alipiga goti kumpongeza Usky, ingawa baadaye alimwaga machozi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
Baada ya ushindi huo, Usyk mwenye umri wa miaka, 35 alisema anataka kuongeza taji la WBC analoshikilia Muingereza mwingine, Tyson Fury zaidi ya hapo hatapigana tena akifikisha rekodi ya kushinda mapambano yake yote 20, kati ya hayo 13 kwa Knockout (KO).
Hili ni pambano la tatu Joshua mwenye umri wa miaka 32 anapoteza, mawili akipigwa na Usyk pamoja na lile la Septemba 25 mwaka jana na moja na Mmexico Andy Ruiz Desemba 7, mwaka 2019 pambano pekee alilopigwa KO, raundi ya saba ukumbi wa Madison Square Garden, New York nchini Marekani.
Joshua ameshinda mapambano 24, kati ya hayo 22 kwa KO likiwemo la marudiano na Ruiz Saudi Arabia Desemba 7, mwaka 2019.
0 comments:
Post a Comment