• HABARI MPYA

        Monday, August 15, 2022

        TIMU NNE KUWANIA NGAO YA JAMII KUANZIA MWAKANI


        BODI ya Ligi imefanya marekebisho ya kanuni kadhaa ikiwemo ya mchezo wa Ngao ya Jamii sasa kushirikisha timu  nne.
        Taarifa ya Bodi imesema timu tatu zilizomaliza nafasi ya juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara zitaungama na bingwa wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) katika shindano hilo.
        Lakini kama bingwa wa ASFC atakuwa miongoni mwa timu zilizomaliza nafasi tatu za juu kwenye Ligi Kuu, basi mshindi wa nne wa Ligi hiyo pia atashiriki Ngao ya Jamii.




        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TIMU NNE KUWANIA NGAO YA JAMII KUANZIA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry