KAMPUNI ya kubasishiri ya Parimatch na uongozi wa klabu ya Mbeya City, imesaini mkataba wa udhamini kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara. Afisa Habari wa Parimatch, Ismail Mohamed, alisema kuwa kampuni ya inayoendesha shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni, leo imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Mbeya City inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara. Alisema kuwa hii mara ya pili kwa kampuni yao kudhamini Mbeya City, hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na Ushawishi na ndiyo kurejea kwao kufanya udhamini. na kutoa vifaa vya michezo na kufanya ukarabati uwanja wa Sokoine. Alisema kuwa Kampuni ya Parimatch moja ya jukumu lao michezo inakuwa kuanzia ngazi ya chini mpaka Kimataifa. Mohamed alisema wameamua kuunga mkono Mbeya City, ili wapenzi wa soka waendelee kupata burudani stahiki. Mohamed Ismail alisema katika udhamini huo wa msimu mmoja Parimatch inatoa pesa taslim, vifaa kwa ajili ya klabu pamoja na ukarabati wa Uwanja wa Sokoine, hasa katika eneo la kukaa bench la ufundi. " Parimatch licha ya kuidhamini Mbeya City, ambayo inashiriki ligi Kuu Tanzania Bara, pia tunaidhamini Chelsea na Leicester City ambazo zinashiriki ligi ya Uingereza"Alisema Mohamed. Afisa huyo wa Habari alisema kuwa anawashukuru Wadau was soka. nchini ikiwa ni pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na bodi ya michezo michezo na Mbeya City kwa kuwapokea kama waday rasmi wa michezo. Mtendaji Mkuu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema kwa upande wao wamefurahishwa na udhamini huo ambao utazidi kuipa chachu ya kufanya vizuri zaidi kwenye msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 15. Alisema Parimatch waliwadhamini msimu wa 2020/21 hivyo kurudi kwao msimu huu, kumetokana na kuridhishwa kwao na udhamini huo uliopita.
"Tunashukuru kwa kupata udhamini huu, maana bado wanaendelea kutumiani, tulikuwa nao wameridhika na kutupa tena nafasi nyingine, tuna imani kubwa ya kufanya vizuri kupitia udhamini huu" Alisema Kimbe.
0 comments:
Post a Comment