• HABARI MPYA

        Tuesday, August 16, 2022

        DIARRA HATIHATI KUIKOSA POLISI TANZANIA LEO


        KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu ya NBC baina ya Polisi Tanzania na Mabingwa wa soka la Tanzania msimu wa 2021/2022 Young Africa Golikipa namba moja wa timu hiyo Djigui Diara huenda akakosekana katika kikosi hicho kuwavaa polisi Tanzania hii leo majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sheikh  Amri Abeid jijini Arusha
        Hayo yamesemwa na Kocha mkuu waa timu hiyo Nasreddine Nabi ambaye ameeleza kuwa Diarra anasumbuliwa na maumivu aliyoyapata kwenye mchezo wa Ngao ya jamii baada ya kugongana na kiungo mshambuliaji kutoka simba Pape Sakho katika harakati za uokoaji wa mpira
        Ameongeza kuwa mbali na mlinda mlango huyo pia Lomalisa Joyce alikuwa na maumivu kidogo hivyo ushiriki wao katika mchezo wa leo unategemea  maendeleo yao katika mzoezi ya leo na ushauri kutoka kwa madkitari.
        Akizungumzia kuhusu mchezo wa leo amesema kuwa polisi Tanzania ni timu ngumu hivyo amewaomba wachezaji wake kusahau ushindi waliopata katika Ngao ya jamii na kuangalia mchezo wa leo ili kupata ushindi kama ilivyo malengo yao ya msimu huu.
        Kwa upande wa kubashiri Kampuni bora ya Kubeti Tanzania Sokabet inakua nafasi ya kubashiri michezo yote ya ligi kuu pamoja na ligi za nje kwa wepesi zaidi tembelea tovuti ya Sokabet au piga *149*35# kujiunga sasa.
        Katika kubashiri Sokabet  inakupa machaguo zaidi ya 400 katika mechi moja, unaweza bashiri umiliki wa mpira, kona za michezo, mfungaji wa bao na machaguo mengine mengi yapo sokabet pekee Kufaidi na kunufaika na ubashiri wako tumia Sokabe best Sports Betting Tanzania.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: DIARRA HATIHATI KUIKOSA POLISI TANZANIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry