BONDIA, Kassim Mbundwike usiku wa jana amekuwa Mtanzania wa pili wa Tanzania kuingia Robo Fainali katika Ndondi Michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea Jijini Birmingham nchini England baada ya kumshinda Pafio wa Cyprus kwa pointi.
Ikimbukwe juzi, Yusuph Changalawe alikuwa wa kwanza wa kutinga Robo Fainali ngumi za ridhaa uzito wa Light Heavy (kg 75-80) baada ya kumshinda kwa pointi Curlin Richardson wa Visiwa vya Anguila.
Baada ya ushindi huo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amempongeza Mbundwike kwa mafanikio hayo.
Akizungumza kwa njia ya simu usiku wa Julai 2, 2022 amesema bondia huyo anastahili pongezi kwa kuwa ameliwakilisha vema taifa na kuwataka wachezaji wote kuiga mfano huo.
Aidha, amesema watanzania wanataka medali hivyo kila mchezaji anapaswa kutanguliza mbele uzalendo wa taifa lake kwa kufanya vizuri.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kusaidia wanamichezo wanaofanya vizuri ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ambaye amekuwa timu nzima amesema kwa sasa wachezaji wana ari kubwa hivyo watafanya vizuri katika michezo iliyosalia.
0 comments:
Post a Comment