Mutambala anajiunga na Yanga kutoka klabu ya Sagrada Esperança ya Angola ambayo alijiunga nayo mwaka 2020 akitokea Excel Mouscron ya Ubelgiji, iliyomnunua mwaka 2017 kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa iliyomuibua mwaka 2013.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 anakuwa mchezaji mpya wa nne Yanga baada ya kiungo Mrundi, Gael Bigiriamana kutoka Glentoran ya Ireland Kaskazini, winga Mghana, Bernard Morrison kutoka Simba na mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Anaungana na wachezaji wenzake Wakongo sita, beki Djuma Shabani, kiungo Yanick Bangala, winga Jesus Moloko na washambuliaji Chico Ushindi, Fiston Mayele na Heritier Makambo.
0 comments:
Post a Comment