TIMU ya Singida Big Stars imemsajili kipa Benedict Haule kutoka Azam FC, ikiwa ni mwendelezo wa kuunda kikosi imara kuelekea msimu ujao.
Haule anakuwa mchezaji mpya wa saba kutambulishwa SBS baada ya kipa mwenzake, Metacha Mnata kutoka Polisi Tanzania na wachezaji wa ndani, Said Hamisi Ndemla kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United, Aziz Andambwile kutoka Mbeya City, Paul Godfrey ‘Boxer’ kutoka Yanga na Kelvin Sabato kutoka Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment