TIMU ya taifa ya Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Morocco 2-1 jana Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.
Shujaa wa Banyana Banyana alikuwa ni mshambuliaji Hildah Magaia aliyefunga mabao yote mawili ya timu yake dakika ya 63 na 71, huku bao pekee la wenyeji, Morocco 2-1 likifungwa na Rosella Ayane dakika ya 80.
Hilo linakuwa taji la kwanza kabisa la WAFCON kwa Banyana Banyana.
0 comments:
Post a Comment