SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiagiza Wydad Athletic ya Morocco kumlipa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva zaidi ya Dola za Kimarekani 700,000 (Tsh. zaidi ya bilioni 1.6).
Hatua hiyo inafuatia Msuva kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya mabingwa hao wa Afrika.
Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake Desemba mwaka jana kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili.
0 comments:
Post a Comment