TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kundi D Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mechi nyingine ya Kundi hilo, Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Geita Gold.
Mechi nyingine za leo ni za Kundi B, ambazo mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wameshinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku Dodoma Jiji ikitoka sare ya 0-0 na Mbeya Kwanza.
0 comments:
Post a Comment