FAINALI ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 itazikutanisha Mbeya Kwanza ya Mbeya na Mtibwa Sugar ya Morogoro Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hiyo ni baada ya timu hizi kuzitupa nje, Azam na Coastal Union katika mechi za Nusu Fainali leo hapo hapo Azam Complex.
Ilianza Mbeya Kwanza kuitupa nje Coastal Union kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Joel Mwambungu dakika ya 83.
Ikifuatia Mtibwa Sugar kuitoa Azam kwa penalti 9-8 baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
0 comments:
Post a Comment