// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAZIRI GEKUL ASHIRIKI MICHEZO YA YOGA UHURU NA KUSEMA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAZIRI GEKUL ASHIRIKI MICHEZO YA YOGA UHURU NA KUSEMA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 19, 2022

    WAZIRI GEKUL ASHIRIKI MICHEZO YA YOGA UHURU NA KUSEMA...


    NAIBU Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inajali kila kitu kinachomwezesha Mtanzania kuishi kwa amani huku akishiriki Michezo na Burudani kwa kadri ya uwezo wake.
    Naibu Waziri Gekul amesema hayo leo Juni 19, 2022 alipowaongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika maadhimisho ya nane ya siku ya YOGA kimataifa yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru, ambapo amesema mazoezi ya YOGA yameonekana kuwa na manufaa sana yanapofanyika kwa utaratibu na utaalamu kiasi cha kutibu na kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
    “Ndugu washiriki, nitumie nafasi hii kuwataka watanzania kuyachukulia mazoezi ya YOGA kwa umuhimu wake ili waweze kujenga umoja, mshikamano na kuboresha afya za mwili na akili pamoja na kusaidia kupunguza msongo wa mawazo" amesisistiza Mama Gekul.
    Naye Balozi wa India nchini Tanzania  Srikanta Pradhan ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa bega kwa bega katika maadhimisho yote yaliyofanyika nchini Tanzania tangu Umoja wa Mataifa kupitia UNESCO kuitambua siku ya YOGA duniani, mnamo Desemba 11, mwaka 2014.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI GEKUL ASHIRIKI MICHEZO YA YOGA UHURU NA KUSEMA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top