TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, wahamaji Niger Uwanja wa L'Amitié Jijini Cotonou nchini katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast.
Tafa Stars ilitangulia kwa bao la mshambuliaji George Mpole wa Geita Gold nyumbani dakika ya kwanza tu akimalizia mpira uliotemwa na kipa Naim-Nhour Jan Van Attenhoven kufuatia krosi ya winga wa Wydad Athletic ya Morocco, Simon Msuva.
Lakini mshambuliaji wa Isloch ya Belarus, Daniel Sosah akaisawazishia Niger dakika ya 26 akimalizia pasi ya beki wa Monastir ya Tunisia, Youssouf Oumarou Alio.
Mechi nyingine ya kundi F, wenyeji Algeria waliichapa Uganda 2-0, mabao ya A. Mandi dakika ya 28 na Y. Belaïli dakika ya 80 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
Mechi zijazo, Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Algeria Jijini Dar es Salaam na The Cranes watawakaribisha Niger Jijini Kampala Jumatano.

0 comments:
Post a Comment