• HABARI MPYA

        Wednesday, June 29, 2022

        NOVATUS DISMAS AJIUNGA NA SV WEREGEM YA UBELGIJI


        KIUNGO chipukizi Mtanzania, Novatus Dismas Miroshi amejiunga na klabu ya SV Zulte Waregem ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
        Miroshi amesaini mkataba wa kujiunga na SV Zulte Waregem jana, akitokea Beitar Tel Aviv Bat Yam alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Maccabi Tel Aviv, zote za Israel.
        Kisoka, Miroshi aliibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kutolewa kwa mkopo Biashara United akapate uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ambako msimu wake wa kwanza tu alipata nafasi ya kwenda Israel.


        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: NOVATUS DISMAS AJIUNGA NA SV WEREGEM YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry