KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Idd Suleiman 'Nado' anatarajiwa kurejea uwanjani mwanzoni mwa msimu ujao baada ya kuwa nje tangu Novemba 30 mwaka jana.
Taarifa ya Azam FC imesema FC Nado aliyeumia dakika ya 29 tu kwenye mechi na Mtibwa Sugar anaendelea vyema baada ya kuanza programu ya mazoezi mapesi kabla ya kurejea dimbani kucheza tena soka la ushindani.
Daktari Mkuu wa Azam FC, Dk. Mwanandi Mwankemwa, amethibitisha kuwa Nado atarejea dimbani kwa soka la ushindani Septemba mwaka huu.
Aidha, Mwankemwa amesema Nado ataruhusiwa kuanza mazoezi na wenzake, wakati Azam FC itakapoanza maandalizi rasmi ya kujiandaa na msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment