WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania inakwenda kushirikiana na klabu ya Southampton ya England kuwandaa makocha wa soka ili wawe kwenye kiwango cha kimataifa.
Waziri Mchengerwa amesema haya juni 17, 2022 ofisini kwake akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk. Hassan Abbasi wakati alipokutana na ujumbe wa Southampton ulioongozwa na Afisa Biashara Mkuu wa Klabu hiyo David Thomas.
Amesema dhamira ya Serikali ni kuona kuwa michezo mbalimbali inasimamiwa kisayansi ili kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwa na makocha ambao watasaidia kufundisha timu za micherzo ili kufuka kwenye kiwango cha kimataifa.
Katika kikao hicho wamekubalina kuwa Timu ya soka ya ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) itakwenda kupatiwa mafunzo maalum kwenye Klabu hiyo ikiwa ni maandalizi ya kwenda kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini Uturuki.
Katika tukio hilo ujumbe wa timu hiyo ulimzawadia jezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kuthamini mchango wake mkubwa anaoutoa kuendeleza michezo nchini.
0 comments:
Post a Comment