TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakwenda Benin kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
Taarifa ya TFF imesema kutakuwa na nafasi 50 kwa wapenzi wa soka watakaotaka kwenda kuisapoti Taifa Stars ambao watalazimika kulipiadola za Kimarekani 1,000 – kwa taarifa Zaidi wafike TFF.
Baada ya hapo, Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
Bahati nzuri kwa Stars, mshambuliaji wa mabingwa wa England, Manchester City, Riyad Mahrez, Said Benrahma na Sofiane Feghouli hawatakuwepo kwa mujibu wa kocha wa Algeria, Djamal Belmadi wote majeruhi.
Ikumbukwe Stars pia itaanzia ugenini kwa Somalia kati ya Julai 22 na 24 kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria, kabla ya timu hizo kurudiana Tanzania kati ya Julai 29 na 31 nchini na mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba.
0 comments:
Post a Comment