WAKATI leo inateremka Uwanja wa Molineux huko West Midlands kumenyana na wenyeji, Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya Englnd – klabu ya Manchester City imekubali kumsajili mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland.
Haaland mwenye umri wa miaka 21, atajiunga na timu hiyo Julai 1 kwa mkataba wa miaka mitano na dau la Pauni Milioni 51 kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani na atakuwa analipwa Pauni 385,000 kwa wiki ili akazibe pengo la Muargentina, Sergio Aguero aliyeondoka msimu uliopita.
Haaland, kwa pamoja na Mfaransa Kylian Mbappe, Haaland ni mwanasoka anayeongoza kwenye kizazi kipya cha nyota wa kabumbu wanaowania kurithi utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Ni mrefu, mwenye nguvu na centre-forward mwenye kasi, ambaye amefunga mabao 85 katika mechi 88 alizocheza Dortmund tangu ajiunge nayo kutoka Salzburg ya Austria Januari mwaka 2020 ambaye pia amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid.
Haaland anatarajiwa kwenda kumuongezea nguvu kocha Pep Guardiola atomize ndoto za kutwaa taji la Champions League, ambalo licha ya kushaili nyota wa gharama kubwa ameshindwa kuipa Man City inayomilikiwa na mabilionea wa Abu Dhabi.

0 comments:
Post a Comment