KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Nassredine Nabi, amesema kesho hawata waachia simba nafasi ya kutinga fainali kwani msimu huu malengo yao ni ubingwa wa Kombe la Shirukisho la Azam ( ASFC) .
Yanga wanashuka katika dimba la CCM Kirumba saa Tisa Alasiri, kuvaana na mabingwa watetezi wakombe hilo Wekundu wa Msimbazi Simba SC.
Watani wajadi hao kwa msimu huu walikutana mara ya mwisho Mei 30 katika mchezo wa Ligi Kuu nakushindwa kuonuonyeshana umwamba kwakumaliza mchezo huo kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Bin Zubery leo katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Mkoani Mwanza, Kocha Nabi alisema kesho hawata bweteka katika kulipambania nafasi ya kutinga fainali ya ASFC.
Alisema mchezo huo nitofauti kabisa namchezo wa ligi hivyo wataingia kwa tahadhari na malengo yao yakiwa nikuwafunga wapinzani wao.
"Tutaingia Kwa tahadhari maana mchezo huu nitofauti nawaligi kwahiyo nia namalengo yetu nikupata ushindi mechi hii ndio funguo ya kwenda fainali lazima tupambane, " alisema
Kwa upande wake kocha wa simba Pablo Martin, alisema Yanga wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini yeye amejipanga na baadhi yawachezaji wake ambao walikuwa maheruhi wamerudi nawatajiunga nakikosi kesho.
Alisema hawezi kuwataja wachezaji hao kwani atakuwa anataja silaha kwa maadui lakini mchezo utakuwa mgumu nawatajitahidi kupambana kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
" mchezo nimgumu na Yanga wanaonekana kama wana nafasi kubwa yakushinda lakini sisi tupo kamili natutajitahidi tuweze kuingia katika fainali kuutetea ubingwa, " alisema.
0 comments:
Post a Comment