MAGWIJI wa soka kutoka sehemu mbalimbali Afrika wamehudhuria sherehe za gwiji wa soka Cameroon, Albert Roger Milla kutimiza miaka 70.
Gwiji Milla alitimiza miaka 70 Ijumaa ya Mei 20, lakini sherehe yake ilifanyika Jumamosi Mei 21 Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde ilipochezwa mechi maalum baina ya magwiji wa Afrika dhidi ya magwiji wa Indomitable Lions.
Timu ya Magwiji wa Cameroon iliundwa na Vincent Ongandzi, Joseph Antoine Bell, Geremie Njitap, Bill Tchato, Jean II Makoun, Bertin Ebwelle, Thomas Libiih, Nicolas Alnoudji, Roger Milla na wengineo.
Timu ya magwiji wa Afrika iliundwa na mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Cameroon, Nchout Njoya Ajara, Rais wa FECAFOOT, Samuel Eto'o, El hadj Diouf, Tresor Lua Lua, Kalilou Fadiga, Alioum Boukar Emmanuel Eboue, Stéphane Mbia na Achilles Emana.
Achilles Emana, Stephane Mbia, Emmanuel Eboue, Nchout Njoya Ajara na mshambuliaji wa zamani wa Portsmouth na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tresor Lua Lua wote walifunga Magwiji wa Afrika wakishinda 6-3 dhidi ya Magwiji wa Cameroon ambao mabao yao yalifungwa na Nicolas Anoudji, Jean II Makoun na 'birthday boy' Roger Milla.

0 comments:
Post a Comment