TIMU ya RSB Berkane ya Morocco imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini Kusini usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria.
Baada ya dakika 90 kumalizika bila mabao, katika dakika 30 za nyongeza Berkane walitangulia na bao la Youssef Elfahli kwa penalti dakika ya 97, kabla ya Thembinkosi Lorch kuisawazishia Orlando Pirates dakika ya 117.
Na kwenye mikwaju ya penalti, Lorch ndiye aliyekosa tuta la pili tu la Orlando huku wenzake wote wanne, Happy Jele, Tshegofatso Mabasa, Thabang Monare na kipa Richard Ofori wakifunga.
Waliofunga penalti za RSB Berkane zilifungwa na Hamza El Moussaoui, Youssef Zghoudi, Ismail Mokadem, Issoufou Dayo na Brahim El Bahraoui.
Katika mchezo huo, winga wa zamani wa Yanga, Tuisila Kisinda alitokea benchi dakika ya 108 kwenda kuchukua nafasi ya Mkongo mwenzake, Chadrack Muzungu Lukombe.
Unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Mkongo, Jean-Florent Ikwange Ibengé aliyejiunga na Berkane Julai mwaka jana baada ya kuachana na timu ya taifa ya nchini mwake.
0 comments:
Post a Comment