VIGOGO, wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 17 na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 39, wakati la Namungo limefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 33.
Yanga inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 20 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi, wakati Namungo inabaki na pointi zake 29 za mechi 21 sasa nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment