WENYEJI, wahamiaji Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mabao ya Mbeya Kwanza leo yamefungwa na Hamisi Kanduru dakika ya 26 na Willy Edgar dakika ya 90 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 21, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16, ikizidiwa pointi moja na ndugu zao, Tanzania Prisons ya Mbeya nayo, ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Coastal Union baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 21 na kushukia nafasi ya 14.
Mbali ya timu mbili kushuka moja kwa moja mwishoni mwa msimu, mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment