MABINGWA watetezi, Manchester City jana walipata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin de Bruyne dakika ya tano na Ilkay Gundogan dakika ya 25 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi
73 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool, baada y wote kucheza mechi 30.
0 comments:
Post a Comment