KLABU ya Manchester United imemuajiri Erik ten Hag kama kocha wake Mkuu mpya wa tano ndani ya miaka tisa, Mholanzi atajiunga na Mashetani Wekundu baada ya kumaliza majukumu yake Ajax mwishoni mwa msimu.
Ten Hag amesaini mkataba wa hadi 2025 jukumu lake kubwa likiwa ni kurejesha mafanikio yaliyopotea United tangu kustaafu kwa Alex Ferguson mwaka 2013 wakati ambao klabu ilishinda mataji yake ya mwisho ya rekodi England, 20.
United imeongozwa na makocha wawili wa muda- Michael Carrick na Mjerumani wa sasa, Ralf Rangnick – tangu kuondoka kwa Ole Gunnar Solskjaer aliyefukuzwa Novemba.
Ten Hag anakabiliwa na kibaruwa kigumu cha kuiumba upya United iwe tishio, baada ya kuachwa mbali na wapinzani, Manchester City na Liverpool licha ya klabu hiyo kuendelea kutumia fedha nyingi kusajili wachezaji.
0 comments:
Post a Comment