SHABIKI wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam na Arsenal ya England, Swalehe Enzi ameshinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.
Enzi ambaye ni mkazi wa Mtwara ameshinda kiasi kikubwa cha fedha hizo baada ya kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za soka za ligi mbalimbali duniani kwa kutumia sh1,000 tu.
Alisema kuwa amebashiri kwa kipindi cha miaka mitatu huku akishinda kiasi cha fedha kidogokidogo ambazo hazikumkatisha tamaa.
Alisema kuwa pamoja na yeye kuwa shabiki wa Simba na Arsenal, bado huwa anakumbana na vipingamizi vingi katika kubashiri kwake jambo ambalo limekuwa kimwaribia ‘mkeka’ wake na ‘kuchanika’.
Shabiki wa klabu ya Simba na Arsenal Swalehe Enzi akipozi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi kwa kushinda Sh176,470,910 kupitia mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania. Enzi alibashiri kwa usahihi matokeo ya mechi12 mbalimbali za mpira wa miguu duniani kwa gharama y ash 1,000 tu.
“Mimi ni fundi selemala na nimekuwa nikibashiri kwa kutumia madaftari au ‘counterbook’. Nimefanya hivyo kwa miaa mitatu huku nikishinda zawadi za fedga ndog ndogo.
Sikuweza kukata tamaa kwani nimeshuhudia washindi kadhaa kupitia Perfect12 ya M-BET wakishinda fedha mamilioni. Nilijua ipo siku name nitashinda kwani hakuna ubabaishaji, natoa wito kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18, kubashiri kupitia M-BET,” alisema Enzi.
Alisema kuwa hakuamini kupigiwa simu kuwa ameshinda kiasi kikubwa cha fedha hicho na sasa kuwa na mipango ya kuendeleza biashara na kuanzisha nyingine, kusomesha na kujenga nyumba.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia mchezo yao.
Mushi alisema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakibashiri na kushinda kupitia michezo yao na kufanikiwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari washindi wamepatikana. Tutaendelea kuwa nyumba za washindi na kubadili maisha ya Watanzania,” alisema Mushi.
0 comments:
Post a Comment