KIKOSI cha timu ya taifa za wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite kimeondoka leo jioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudano na wenyeji kufuzu Kombe la Dunia Ijumaa Jijini Addis Ababa.
Tanzanite ambayo iliweka kambi ya wiki moja akademi ya Black Rhino, Karatu mkoani Manyara - inahitaji sare katika mchezo huo kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Aman, Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment