TIMU ya taifa za wasichana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania. Tanzanite imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Ethiopia katika mchezo wa marudano Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia jioni ya leo Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.
Kwa matokeo hayo, Tanzanite inatolewa kwa jumla ya kichapo cha 2-1 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Aman, Zanzibar.
Sasa Ethiopia itakutana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Ghana, ambao ni mtihani wa mwisho utakaotoa tiketi ya kwenda Costa Rica katika Fainali zitakazoanza Agosti 10 hadi 28, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment