MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Union Sportive Gendarmerie Nationale usiku wa leo Uwanja wa wa Jénérali Seyni Kountché Jijini Niamey nchini Niger katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
Wenyeji, Gendarmerie walitangulia kwa bao la Wilfried Gbeuli dakika ya 12, kabla ya winga Mghana, Bernard Morrison kuisawazishia Simba dakika ya 84.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi nne na kupanda kileleni wakifuatiwa na RS Berkane ya Morocco yenye pointi tatu sawa na ASEC Mimosa ya Ivory Coast, wakati Gendarmerie Leeds inakamilisha mechi mbili bila pointi za inaendelea kushika mkia.
0 comments:
Post a Comment