WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yote yamefungwa na washambuliaji wake Wareno, Cristiano Ronaldo dakika ya 51 na Bruno Fernandes dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Brighton ilimaliza pungufu kufuatia beki wake wa kati, Lewis Dunk kutolwaa kwa nyekundu dakika ya 81 kwa kumchezea rafu Anthony Elanga dakika ya 81.
Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 25 na kupanda nafasi ya nne, wakati Brighton inabaki na pointi zake 33 za mechi 24 sasa katika nafasi ya tisa.
0 comments:
Post a Comment