WENYEJI, Manchester United wametupwa nje ya michuano ya Kombe la FA England baada ya kufungwa kwa penalti 8-7 kufuatia sare ya 1-1 na Middlesbrough usiku wa Ijumaa Uwanja wa Old Trafford.
Nyota Mreno wa Manchester United, Cristiano Ronaldo alikosa penalti dakika ya 20, kabla ya mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kuifungia bao kuongoza Manchester United dakika ya 25 na kiungo, Matt Crooks kuisawazishia Middlesbrough dakika ya 64.
Katika mikwaju ya penalti, Anthony Elanga alikosa penalti ya nane iliyokitupa nje kikosi cha kocha Mjerumani, Ralf Rangnick katika Raundi ya Nne Kombe la FA mbele ya timu ya Championship, Middlesbrough.
0 comments:
Post a Comment